ABSTRACT
Ikisiri
Hotuba ni usemi unaotolewa kwa hadhira kwa njia ya mazungumzo au maandishi kwa uzingatifu wa jambo mahsusi. Miongoni mwa maraisi wa nchi huwa mna waliojaaliwa vipaji vya kiuneni kiasi cha kuwafanya raia wa nchi zao kuyaamini yale wayasemayo na kuyaingiza katika utendaji wa maisha ya kila siku; mintaarafu ni Mwalimu Nyerere; hotuba zake zimegubika lugha makbuli ya Kiswahili. Mwalimu Nyerere alipendelea Kiswahili kitumike katika siasa za kiafrika badala ya lugha nyingine yeyote ya Ulaya kwa uoni kwamba kuendeleza lugha zao si tu kwamba ni kuukumbatia utumwa lakini kuuza utu wa Mwafrika – Bloommaert, 1990. Hotuba zake daima zimekuwa ni mshawasha kwa wasomaji na wasikilizaji kila uchao; hasa kwa jinsi zilivyo tagaza ufahima hususani katika kila nyanja ya maisha ya mwanadamu. Leo yake Mwalimu Nyerere hatunaye tena. Makala haya yameongozwa kwa nadharia ya Balagha (Rhetoric Theory); na madhumuni yake makuu ni kubainisha mbinu za kifani alizozitumia Mwalimu Nyerere kuendeleza maudhui yake kupitia hotuba zake hata ikawa ni abakie katika vinywa vya watu wengi, wakimlilia hadi hivi leo.
Maneno muhimu: ushawishi wa hotuba za Mwalimu Nyerere, Kiswahili